Ugumu
wa game la muziki nchini umewafanya wasanii wengi kubuni njia mbadala
(za kimafia zaidi) kutengeneza ‘keek’ mjini kama wasemavyo vijana wa
siku hizi.
Wengine wamewahi kusambaza picha za uongo kuwa walikamatwa na madawa
ya kulevya ili kuitengenezea njia nzuri ngoma mpya,(sikumbuki kama stunt
hii ilifanikiwa, I guess it flopped). Wengine huyatumia magazeti
kutengeneza stunts za kila aina ilimradi tu majina yao yasitoke midomoni
mwa mashabiki wa muziki. Njia hii imewasaidia wengi lakini wengine
stunts zao ziki’backfire’ na kuwaletea timbwili la kufa mtu mtaani.
So katika muendelezo huo wa kutafuta keek mjini, rapper Baghdad
ameamua kuwa ‘kreative’ kidogo. Vipi kama ukiwasikia maadui wawili
kimuziki ambao ni kama Paka na Panya kwenye ngoma yake? Inasound poa
sio? Rapper huyo ameamua kucheza mchezo ‘mchafu’ kwa kuwakutanisha Nay
wa Mitego na Chidi Benz wenye beef bila wao kujua.
Alichofanya Baghdad ni kuwaambia kila rapper katika muda wake kuwa
angependa kumshirikisha. Nay wa Mitego alipewa kazi ya kuipamba chorus
ya ngoma hiyo iitwayo ‘Waambie Nipo’. Nay bila kinyongo aliingiza sauti
zake na mwisho kuweka outro. Kwenye outro Nay anasikika akisema
‘mngenipa hata verse moja tu niwaharibie humu, mna bahati’
Chidi Benz kwa muda wake naye aliingiza verse ya pili kwenye ngoma
hiyo bila kujua kuwa adui yake Nay kapita kwenye chorus ya ngoma hiyo.
Wasanii hao wawili wamekuja kufahamu mchongo huo jana baada ya kupigiwa
simu na Gossip Cop kwenye U Heard ya Clouds ambapo wote waliipokea
habari hiyo kwa surprise kubwa.
Nay alichukia kwanini Baghdad hakumwambia kuwa Chidi pia atakuwemo
humo na kwamba hata kama angemwambia ukweli asingekataa kufanya kwakuwa
yeye ni mfanyabiashara. Hatua hiyo imemfanya Nay akatae tena kuendelea
kufanya video ya wimbo huo licha ya kuwa tayari alishashoot baadhi ya
vipande.
Hata hivyo Chidi Benz habari hii aliipokea kwa jaziba na kumtaka
Baghdad aitoe verse yake kwenye wimbo huo, jambo ambalo halijafanyika
kwakuwa tayari wimbo umetoka. Kwa lugha rahisi ni kwamba Baghdad
kaharibu kwa rappers wote na huenda wameshampigia simu kumchimba mkwara.
Unakionaje kitendo hicho cha Baghdad kuwakutanisha maadui kwenye wimbo
wake bila wao kujua?



