Rappe Ney wa Mitego, kupitia wimbo wa "Nasema nao" alifanikiwa kupata tuzo ya
wimbo bora wa hiphop, ambao umesababisha malalamiko kwa baadhi ya
wasanii wengine ambao wnaona hakustahili kuchukua tuzo hiyo kwa wimbo
huo, huku wengine wakidai Fid q anastahili na wengine kudai Stamina ndio
anastahili....leo hii Ney mwenyewe kafunga juu ya swala hilo
"aah
wasanii ndio wanaolalamika na wameandika kwenye mitandao, lakini mwisho
wa siku lazima tukubali matokeo kwamba mziki unabadilika kila kukicha,
mi nawaambia wasanii wenzangu kwamba mkiendelea kung'ang'ania huko
mtakufa njaa, halafu mwisho wa siku wataendelea kulia tu kila siku
kwamba kuna hili mara lile,mi naimani kwamba mashabiki wangu ndio
wamenikabidhi tuzo, media zinazosapoti kazi yangu ndio zimenisaidia
mpaka mimi nimezungumza na mshabiki wangu popote walipo mpaka juzi
nimepata tuzo ya wimbo bora wa hiphop. mi nastahili kupata tuzo,
kwasababu kwanza sijui wao wanafanya hiphop gani, wakae waeleze mziki
wao wao ni hiphop kwasababu hii na hii na hii na wangu sio hio hiphop
kwasababu hii na hii na hii. bwana hiphop ni ukweli na unabadilika kila
siku kila kukicha. Mi nawashauri tu kitu kimoja, sitaki kubishana na
msanii yoyote, wana njaa, wakiendelea kung'ang'ania huko watakufa njaa,
kwanini watu wamemsapoti Ney, kwanini watu wamemsapoti Kala
Jeremiah,angalia mashairi ya Kala yako wazi, lakini we unaweka sijui
mafumbo ya dizaini gani nani atakuelewa...........
halafu
tuzo sio lazima upate tuzo, sio lazima ulaumu, kuna wasanii wakali
hawajawahi kupata tuzo lakini hawajawahi kulalamika, kuna wasanii kama
Juma Nature, nani anaweza kusimama stage na Nature? sijawahi kumsikia
anaongea.....
category
moja tu nimewekwa nimetusua wao wanalia, shauri yenu shauri yenu,
jipangeni mwakani, mi staki kubishana nao, am the best, halafu
wasipoangalia nawatengenezea kiwanda kwa ajili ya kuwaajiri
wanapoendelea kuwana na hali ngumu, natengeneza kiwanda ambacho
ntawaajiri wasanii wanaofeli wote kwasababu hawana shughuli za kufanya." amesea Ney.
Credit: audifacejackson.blogspot.com