Release No. 098
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 11, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 11, 2013
Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Algeria
kuchezesha mechi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayofanyika
Jumapili saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kundi C kuwania tiketi ya
kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil wataongozwa na
Charef Mehdi Abid atakayepuliza filimbi. Atasaidiwa na Hamza Hammou na
Bouabdallah Omari wakati mezani atakuwa Sofiane Bousseter.
Abdi na wezake wanatarajiwa kutua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu)
saa 12 asubuhi kwa ndege ya EgyptAir. Mtathmini wa waamuzi ni Athanase
Nkubito kutoka Rwanda ambaye atatua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu)
saa 12 jioni kwa ndege ya RwandAir.
Kamishna wa mechi hiyo ni Bernard Mfubusa kutoka nchini Burundi
ambapo atawasili nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa
ndege ya Kenya Airways. Maofisa wote hao wa mechi hiyo watarejea makwao
Jumatatu (Juni 17 mwaka huu).
Credit: audifacejackson blog