
Hapa akionekana mwenye uvimbe zaidi
Hapa akionyesha majeraha ambayo aliyapata shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyo
Hapa akiwa hoi kwa kipigo
Bi Rehema
Shauri Madongo mkazi wa Wilolesi mjini Iringa akiwa na mtoto wake baada
ya kuponea katika tundu la sindano kuuwawa kwa kipigo kutoka kwa mmewe
ambaye ni askari polisi mjini Iringa kiasi cha kukimbia nyumba na kurudi
kwa wazazi wake
stepen kanyala akiwa na mke wake siku ya harusi yao iliyodumu kwa miaka mitatu sasa
Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri |
IGP Mwema
WAKATI
jeshi la polisi nchini likiendelea kujiweka karibu na Raia hata kuamua
kuanzisha dawati la jinsia katika vituo vya polisi ,kwa mkoa wa Iringa
baadhi ya askari wanadaiwa kupiganga na jitihada hizo za polisi kwa
kushindwa kuheshimu dawati hilo na badala yake kushiriki kulivunjia
heshima jeshi hilo kutokana na kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na
mkakati wa jeshi hilo katika kuanzisha dawa.ti la jinsia.
Uchunguzi
wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com na
www.francisgodwin.blogspot.com umeonyesha kuwa dawati hilo kwa askari
limekosa kuheshimika kutokana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia
ambavyo baadhi ya askari (30) wamekuwa wakifanya kwa watoto wao na wake
zao.
Rehema
Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na
askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa
vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi
anapofika polisi hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo
ambaye ni askari .
" Mimi
niliolewa kwa ndoa na Stephen Kanyala ambae ni askari kitengo cha
upelelezi ila baada ya kuolewa ukiwa umepita mwezi mmoja tuo nilianza
kushuhudia mateso ya ndoa kutokana na kipigo na mateso makali niliyokuwa
nikiyapata"
Anasema
kuwa kila wakati pindi anapotaka kujua jambo kutokana kwa mume wake huyo
hasa pale anapoona jumbe zenye utata katika simu yake ambazo zimetoka
kwa wanawake anaiowatambua vizuri amekuwa akijibiwa kwa kipigo kikali.
Rehema
alisema kuwa ni rahisi kwake kuweza kuhesabia siku ambazo hajapigwa
kuliko kuhesabi siku ambazo amepigwa ambazo ni nyigi zaidi .
Kwa
alisema toka ameolewa kila mara amekuwa akipokea kipigo na mbaya zaidi
kabla ya kupigwa amekuwa akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika
kuwafunga watuhumiwa pingu ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi
ndani ya nyumba .
" Kweli
inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa
pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa
kikinikuta ....hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda
kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine
nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu
sasa"
Alisema
kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa
akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa
hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa
kinyama.
Hata
hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi
zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka
kunyonga shingo huku akitishi kumuua .
Alisema
kuwa baada ya kujifungua mtoto wa njia ya Oparesheni mwanaume huyo
alimpiga kiasi cha kumjeruhi mtoto wa mwezi mmoja kwa kumpiga kofi
ambalo lilielekezwa kwake na bahati mbaya likaishia kwa mtoto.
Aidha
alisema kuwa kila akifika polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji
unaofanyika kutokana na polisi kulindana na kuwa suala hilo la askari
polisi kulindani lilianza toka wakati kamanda wa polisi akiwa Evarist
Mangala ,pia alipofika kamanda Michael Kamuhanda ambaye kwa sasa
amehamishwa baada ya cheo kupanda pia amepata kufikisha malalamiko yake
ila hakuna jipya ila sasa amefikisha tena suala hilo kwa kamanda mpya
RPC Ramadhan Mungi ambae amedai kuwa na imani nae zaidi katika kulishughulikia suala lake
Pia
alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani kwake ila bado anapoamua
kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi wake bado askari huyo
amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi wake .
Hivyo alisema katika kunusuru uhai wake kwa sasa ameamua kurudi kwa wazazi wake na suala la ndoa hataki tena .
Kwa
upande wake Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri alisema kuwa
amechoka kuuguza binti yake kwa kipigo na kuwa kuna wakati mwanaume huyo
amekuwa akitishia kumpiga hata yeye.
Hivyo
alisema kwa sasa mbali ya kumtoa binti yake Hospital ila wamekuwa
wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia
ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa
akiwatisha mara kwa mara kuwa dawa yao inachemka na ipo siku wataonja
mauti.
Bi Shauri
alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole
mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa
anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo .
Hivyo
aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama
kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa
Iringa ila askari wenzake wanamlinda.
Kuhusu
uamuzi wa binti yake wa kuomba ndoa hiyo kuvunjwa alisema anaungana na
binti yake kuikataa ndoa hiyo na kuwa kwa sasa wapo tayari kurudisha
mahali yake ya Tsh 200,000 ambazo alizitoa kama mahali ili kunusuru uhai
wao na uhai wa mtoto wake huyo.