Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, May 10, 2013

Wateja wa huduma za simu za kutuma na kupokea pesa nchi ya Uganda watalazimika kulipa ada zaidi za kutuma na kupokea pesa


Wateja wa huduma za simu za kutuma na kupokea pesa nchi ya Uganda watalazimika kulipa ada zaidi za kutuma na kupokea pesa baada ya kampuni ya huduma za simu ya MTN kuongeza ada zake. 

Afisa mkuu wa mauzo katika kampuni hii Ernst Fonternel, amesema kwamba wamelazimika kuongeza ada hizo hili kupata fedha za kuboresha huduma zao kwa wateja. 

Ongezeko la ada hizi lilianza kufanya kazi hapo jana na ziliongezeka kati ya shilingi mia moja na elfu mbili za Uganda. 

Huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu zimeendelea kuwa maarufu nchi ya Uganda na pia kote Afrika mashariki. 

Jumla ya pesa zilizotumwa kupitia njia ya simu mwaka uliopita nchi ya Uganda zilifika shilingi trilioni kumi na moja nukta saba kutoka shilingi trilioni tatu nukta saba tano mwaka wa elfu mbili na kumi na moja.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...