Mmoja wa wakazi wa tabata
chang'ombe akiangalia gari dogo aina ya corola iliyowaka moto mara baada
ya fundi aliyekuwa anachomelea huku akiwa hajachomoa betri na kupelekea
kuungua maeneo ya Tabata Chang'ombe
Wakazi wa Tabata Chang'ombe
wakiwa katika jitihada za kuzima gari hilo dogo ambalo limeungua
kutokana na fundi kuchomelea huku akiwa hajatoa betri la gari hilo
maeneo ya Tabata Chang'ombe Mapema asubuhi ya leo
Wakazi wa Tabata Chang'ombe
Wakiangalia gari hilo dogo aina ya corola iliyoungua leo maeneo ya
Tabata Chang'ombe mara baada ya fundi kuchomelea gari hilo huku akiwa
hajachomoa betri na kupelekea kuungua. Picha Zote na Fransisca wa Lukaza
Blog
Gari ndogo aina ya Toyota Corola
imeungua kwa moto mapema leo maeneo ya Tabata Chang'ombe mara baada ya
Fundi aliyekuwa anachomelea kuchomelea gari hilo huku akiwa hajatoa
betri la gari hilo na kupelekea kuwaka moto ambao wakazi na majirani hao
walijitahidi kuuzima kwa maji na mchanga lakini bila mafanikio na
kupelekea gari hilo kugeuka ghafla chuma chakavu.
Gari hilo lilipelekwa na dereva
ambaye aliliacha Kwa fundi huyo katika garage bubu maeneo ya Tabata
Chang'ombe na yeye Kuelekea Kinyerezi kuangalia Shamba lake. Mara baada
ya Kuliacha kwa fundi gari hilo lilianza kufanyiwa matengenezo na
kupelekea Fundi huyo kuchomelea bila kutoa betri na kupelekea kuwaka
moto ambao pamoja na jitihada za wakazi na majirani wa garage bubu hiyo
kujitahidi kuuzima kwa mchanga na maji lakini walifua dafu.
Baada ya Kuonekana anayesemekana
kuwa ni mmiliki wa garage bubu hiyo kuonekana akilia kwa uchungu sana na
kupelekea watu kuhisi kuwa anawaza jinsi ya kulipa gari hilo na ndipo
wadau wakabidi kumuuliza dereva huyo kuhusu gari hilo kama lina bima.
Kwa Mujibu wa Dereva wa gari hilo ambaye ni dereva taksi ameuambia
mtandao wa Lukaza Blog kuwa Gari hiyo ilikua haina bima kwa muda mrefu
na kwahiyo kuungua kwa gari hii kumemfanya kuwa maskini na kupelekea
kumpa mawazo sana.