CHUO
Kikuu cha Kiufundi cha Mombasa (TUM) kimekanusha madai kwamba wanafunzi
wake ni makahaba wanaofanya vitendo vya ngono na mbwa.
Kwenye
barua ya kukana dai hilo iliyopelekwa kwenye vyombo vya habari baada ya
chuo hicho kutajwa kama chenye wanafunzi 11 waliokamatwa Nyali juzi kwa
kashfa ya ngono, chuo hicho kilisema kina mikakati mikali ya kufundisha
maadili.
“Tunapenda kusahihisha uongo na kusema ukweli juu ya suala linaloendelea kugonga vichwa vya habari juu ya ngono
za kinyama na mbwa,” ilisema barua hiyo.
Barua
hiyo iliyotiwa sahihi na Naibu Mkuu wa chuo hicho Prof Josphat Mwatelah
ilisema, “Tungependa kuweka wazi kwa wazazi wote na umma kwamba madai
ya watu (wasichana) waliokamatwa wiki jana huko Nyali Mombasa kwa
masuala ya ukahaba na kufanya mapenzi na mbwa kuwa ni wetu ni uongo.
Wasichana hao si wanafunzi wetu wala hawahusiani kivyovyote na chuo
chetu."
Barua
hiyo iliendelea kwamba pekuapekua za stakabadhi za chuo hicho kikuu
hazikuonyesha hata jina moja kwamba ni la mwanafunzi wao.
“Kikosi cha walinda usalama wetu pamoja na
wachunguzi maafisa wa polisi vimethibitisha kwamba watu hao kamwe si
wanafunzi wetu”, ilisisitiza barua hiyo.
Nakala hiyo iliendelea, “Chuo chetu kina
kitengo madhubuti cha kuelekeza wanafunzi na kuwatia nia na maadili mema
ya kijamii. Chuo chetu pia kina kitengo madhubuti cha kuongoza
wanafunzi juu ya maovu yanayokithiri nchini Kenya,” ilisema.
Barua
ilieleza kwamba TUM imejitolea kuendeleza mafunzo bora kwa wanafunzi
wake ili hatimaye wawe wananchi wenye maadili, tabia na mienendomizuri
katika jamii.
“Tunavionya vyombo vya habari kwa kutaja
jina la chuo chetu kuhusiana na kashfa hii na kwa kuharibu jina na sifa
ya chuo chetu pasipo kuthibitisha taarifa yenyewe kwanza na kutaka
vituombe msamaha kupitia umma”, iliongeza barua hiyo.
Suala hiyo limezua mjadala mkali na
kushutumiwa nchini na nchi za ng’ambo huku mashirika ya dini na ya umma
yakitaka uchunguzi kamili na wageni wanaohusika kwenye njama hiyo
wakamatwe, washtakiwe kasha warudishwe makwao hatimaye.
Polisi hapo Jumapili walidokeza kwamba
wanamtafuta mwanamke mmoja kutoka Karatina anayetuhumiwa kuzama kwenye
lindi la biashara hiyo haramu na ambaye ameingia gizani tangu wasichana
hao 11 kukamatwa huko Nyali.