TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA
MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA
LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013
Ndugu
wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi
niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta
maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika
kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe
05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa
kujeruhiwa.
Kama
nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa
tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa
bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa
bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha
bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23)
mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.
Watuhumiwa
wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu
(UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika
falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi
wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28)
askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia
mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)
Rai
hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa
tanzania wenye asili ya Yemen. Majina ya watanzania hao ni Mohamed
Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak
(29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.
Uchunguzi
wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za
upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa
bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika
shambulio hilo.
Baada ya
jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao
wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama
kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati
walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Pia ofisi
ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor S/O
Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji na
kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea kwa
sasa tunao wataalamu kutoka kenya na Uganda ambao tunashirikiana nao
katika upelelezi wa shauri hilo.
Aidha,
hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu
wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao
kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru
arusha, 4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika
hospitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha
hali zao zinaendelea kuimarika.
Hata
hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa
wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa
mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au
raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi
nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha
taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi
zawadi nono ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo
za siri kwa kukamatwa kwa watu hao.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP