Joseph Mbilinyi aka "Sugu"
Joseph Haule aka Proffessor Jay"
Lady Jay Dee mwenyewe
K na D wa Maujanja Saplayaz (Kulwa na Dotto)
WAKATI wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wakisubiri kwa hamu kubwa show kali ya Mwanadada Judith Wambura "Lady Jay Dee" ya
kuadhimisha kutimiza miaka 13 katika game ya Muziki huo na kutokana na
hali ambayo imeendelea kwa baadhi yawasanii mbalimbali waliokuwa
wametajwa kushirikiana naye katika show hiyo kujiengua na kutoa sababu
kadhaa za kutoshiriki katika Show hiyo (TID, Linah, Barnaba na Matonya).
Wapenzi
mbalimbali wa Muziki huo ndani na nje ya nchi wamesikika kutoka katika
sehemu mbalimbali haswa katika mitandao ya kijamii (Facebook na
Tweeter).
Wakishauri
Msanii huyo kuachana na wasanii hao "njaa kali wenye tamaa za muda
mfupi" na kuangalia wasanii wengine wenye kutambua wajibu na kuthamini
haki zao na wasanii wenzao badala ya kuishia kutumika kwa maslahi ya
watu wachache ambao nyuma na hata mbele ya pazia ni hao hao ambao
wamekuwa wakiwakandamiza na kuwanyonya wasanii nchini.
Aidha kwa kutokujua na wengine kukujua lakini kwa kule kuendekeza/kutanguliza njaa mbele.
Pichani juu ni baadhi ya Wasanii ambao baadhi ya wapezi wa Msanii Lady Jay Dee wameomba wahusishwe katika kutoa burudani katika show hiyo ili kuipa makali zaidi