MAMA
wa marehemu Salome Yohana, Pendo Dustan Mushi (picha ndogo katikati)
ambaye kichwa cha mwanaye huyo kinadaiwa kukutwa na Ramadhan Suleiman
‘Rama mla watu’ amezua timbwili Mahakama Kuu, jijini Dar akitaka kujua
hatma ya kesi hiyo ya mauaji.Tukio hilo lilitokea Mei 16, mwaka huu
ambapo mama huyo alinaswa na kamera yetu akilalamika huku akilia kwa
uchungu akitaka kujua hatma ya kesi hiyo ya mwanaye ambayo imedumu tangu
mwaka 2008.
“Nataka kujua hatma ya kesi ya mauaji
ya mwanangu, mara kwa mara nimekuwa nikija hapa mahakamani na kurudi
bila kujua chochote kinachoendelea.
“Inaniuma sana kuona hukumu
haitolewi, licha ya mwanangu kupoteza uhai muda mrefu lakini siwezi
kumsahau, nimekuwa nikilia kila nikikumbuka kifo chake na hasa siku za
kesi ndiyo huwa naumia sana,” alilalamika mama huyo na kuongeza:
“Hata mwenendo mzima wa kesi
siufahamu, nilisikia kwenye vyombo vya habari kuwa kesi yake inasomwa
leo lakini mpaka dakika hii sielewi chochote.”
Baada ya kulalamika sana, mama
huyo alipata msaada wa kufikishwa kwa makarani wa kesi za jinai
mahakamani hapo ambao walimhakikishia kuwa kuwa kesi hiyo itatajwa Mei
24, mwaka huu mbele ya Jaji John Temba wa mahakama hiyo.
Rama ambaye alijizolea umaarufu
mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu
kinachodaiwa kuwa ni cha Salome, hadi sasa anasota Gereza la Segerea
Jijini Dar akisubiri mwenendo wa kesi hiyo