Msanii wa
muziki wa kizazi kipya Chid Beenz, amesema watu wengi wanayafatilia
maisha yake sababu yeye ni msanii mkubwa na ni star zaidi yao.
Chid
ambaye masikani yake ni Ilala Flats jijini Dar, amesema kitendo cha watu
kuwa wanamfatilia kwa yale au kile anachokifanya sababu yeye ni msanii
mkubwa na wasanii wengine inabidi wamfuatilie.
Maoneno
hayo yalikuja baada ya kumuuliza swali juu ya alichokisema Kala Pina,
kwamba Chid ameathiriwa na madawa, ndipo Chid alipojibu,“Sasa yeye
mwenyewe mbona anavuta ganja, vitu kibao anafanya, sasa kwani mbona mimi
simtangazii kwenye media, mimi sina habari, yeye kama ananifatilia
hivyo nashukuru kumbe mimi ni bonge la star.
KUANGALIA VIDEO YA CHID BEENZ AKICHEZEA KICHAPO
Aliendelea
Chid akisema, “Umeona mwandishi watu wanahisi nimepotea, wakati kina
Pina wananifatilia hadi maisha yangu, oohhh navuta nini…., sijui
nimetoboa nini….., nilihisi hajawahi kuniona na kaona nimefanya nini….,
nimevaa niko nini……, kumbe wananiona hivyo hadi nafanya nini, safi
sana…” Alimalizia Chid Beenz…