Maharusi watarajiwa Dimaond Platnumz & VJ Penny |
Esma
Abdul ambae ni dada yake mwimbaji staa wa Tanzania, Diamond Platnums,
amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae
anatarajiwa kumuoa mtangazaji wa TV aitwae Penny.
Esma
ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, "Tumemkubali sana wifi
yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi
nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye
ataniingilia kwenye mapenzi yangu."
Huu ni
mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema nyumbani
amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini
itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa.
Dada yake Diamond aka wifi yake Penny |
Zaidi ya
wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake imekaribia
kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia
akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan -
Hyundai IX 35.
Mpaka
sasa Mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa
Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye
headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma
kama Jokate, Wema Sepetu na wengine.
Source: Millard Ayo
Source: Millard Ayo