.....................................................
Na Juma Nyumayo, Songea
JESHI
la Polisi kwa mara nyingine tena Mwezi huu limekamata Pembe za Tembo
zenye thamani ya shilingi milioni 38,398,000 kutoka mtandao wa majangili
wa Kijiji cha Mandepwende wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, amemuambia mwandishi wa
habari hizi nje ya Ofisi yake kuwa yeye na Kikosi cha kuzuia Ujangili
Kanda ya kusini wamejipanga vizuri na ndio maana Mtandao wa Majangili
umebanwa kila kona. "Nakuambia hawa tutawabana kila kona, maana nakili
kuwa tunafanya kazi kwa uelewano mkubwa na kikosi cha Kuzuia ujangili
kanda ya kusini," alisema Kamanda Nsimeki akitamba kuwa sasa ndio
Arobaini yao.
Alisema
ametoa wito kwa wanchi wema kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na
usalama na pia kuwatahadharisha wote wanaojihusisha na biashara hiyo
waache mara moja. Pembe za ndovu zilizokamatwa ni 11 ambazo ni sawa na
Tembo sita ambao wameuawa na majangili hao.
Hivi
karibuni, jumuia za kimataifa zimelaani biashara ya pembe za tembo
ambazo zimesababisha kuuawa kwa Tembo wengi hapa Afrika. Miongoni mwa
mataifa yanayolaumiwa zaidi ni pamoja na nchi za Afrika Mashariki
Tanzania ikiwa mojawapo.



