KESI ya kutorosha wanafunzi inayomkabili Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG), Jean Felix Bamana, Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jumatatu wiki hii ilianza kurindima katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Kilimanjaro huku upande wa walalamikaji ukiiambia korti, ‘mchungaji alitaka penzi bila kinga’.
Mchungaji huyo alitiwa mbaroni
Machi
13, mwaka huu ndani ya Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni, Dar akiwa na
wanafunzi wawili, watoto wa familia moja, Artha Swai (17) na Angel Swai
(19) ambao alidaiwa kuwatorosha kutoka mjini hapa.
Katika
kesi ya msingi, mchungaji huyo alidaiwa kuwadanganya watoto hao kwamba
alikuwa akiwafanyia mpango wa kwenda kusoma nje ya nchi lakini badala
yake aliwaweka hotelini na kumtaka kimapenzi mmoja wao
SAA 3:30 ASUBUHI AFIKISHWA MAHAKAMANI
Akiwa
chini ya ulinzi mkali wa polisi, Amani lilimshuhudia Mchungaji Bamana
ambaye alishindikana kufikishwa mahakamani mara tatu mfululizo kwa
visingizio vingi, akipandishwa kizimbani huku akikwepa macho ya umati
uliofurika kufuatilia kesi hiyo.
MASHITAKA
Akisoma
mashitaka yanayomkabili Mchungaji Bamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Moshi, mbele ya Hakimu Naomi Mwerinde, mwendesha mashitaka ambaye ni
wakili wa serikali, Abdallah Chavula alisema mtuhumiwa huyo anashitakiwa
kwa makosa mawili.
Chavula
alisema, katika makosa hayo, la msingi ni la kutorosha wanafunzi kinyume
na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya sheria namba 6 ya mwaka
2008, ibara ya 4, kifungu cha 5, kifungu kidogo 4 (i)a.
Katika
mashitaka hayo, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mnamo Februari 18, mwaka
huu, Angel ambaye kipindi hicho alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tano
katika Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Marygorethi ya mkoani hapa,
akiwa nyumbani kwao eneo la Masama wilayani Hai, alimuomba mdogo wake,
Artha amsindikize mjini Moshi.
Mwendesha
mashitaka huyo aliendelea kufafanua mbele ya mahakama hiyo kuwa,
wanafunzi hao waliondoka nyumbani bila kutoa taarifa na kwamba walifikia
Moshi View Hotel ambako walikutana na mshitakiwa huyo.
Ilidaiwa
kortini hapo kuwa wakati watatu hao wakifanya mazungumzo, Artha
alimueleza mshitakiwa dhamira yake ya kuendelea na masomo baada ya
kumaliza kidato cha nne na mtuhumiwa alimhakikishia kwamba kwa kuwa ni
mtu wa kuzuguka kila mahali duniani kote angemsaidia kupata shule nje ya
nchi.
Ilielezwa
kuwa kama ilivyokuwa kwa mdogo wake, Angel naye alihakikishiwa
kufanyiwa utaratibu wa kupata shule nje ya nchi ambapo mshitakiwa
alimuahidi kumpeleka Uingereza kusomea masuala ya ubunifu na mitindo.
Mwendesha
mashitaka huyo aliiambia mahakama kuwa majira ya saa tisa alasiri,
mshitakiwa aliwapa nauli ya teksi kutoka Moshi kuwarudisha nyumbani
Masama na kwa kuwa waliondoka bila kuaga, bibi yao aliwagombeza.
Chavula
aliendelea kuiambia mahakama kuwa, katika mawasiliano kati ya watatu
hao, Mchungaji Bamana alikuwa akimsisitiza Angel afanye uamuzi mgumu wa
kuondoka nyumbani kwao na kumfuata Dar kwa sababu wazazi wake (Angel),
watakufa muda wowote, yeye na mdogo wake watapata matatizo kama watakuwa
hawawezi kujitegemea.
ZAWADI YA SIMU
Mahakama
iliendelea kuelezwa kuwa siku ya kwanza kukutana, mshitakiwa alimpa
Artha simu ya Samsung Touch Screen na kwamba siku iliyofuata, mtuhumiwa
alimpigia simu Angel kupitia simu aliyompa Artha na kuwataka waende
mjini wakale naye bata.
Angel na
mdogo wake walitoroka nyumbani kwa kutumia usafiri wa teksi ya mtu
aliyefahamika kwa jina moja la Yusuf ambapo baada ya kufika mjini
walikutana na mchungaji huyo aambaye aliwapeleka Nakumatt Supermarket
alipowanunulia biskuti na headphone za simu.
SMS ZA MAPENZI
Mahakama
ilielezwa kuwa, pande zote ziliendelea kupigiana simu na kutumiana
ujumbe mfupi (SMS) na katika mazungumzo, mshitakiwa aliendelea
kuwasisitiza Angel na Artha kutoroka nyumbani na kuongeza kuwa siku
iliyofuata mshitakiwa aliondoka kurejea Dar.
ARTHA AMFUATA MCHUNGAJI DAR
Hakimu
Mwerinde aliambiwa kuwa, Februari 18, mwaka huu, Artha alimuaga baba
yake kuwa anakwenda Machame kumsalimia bibi yake lakini badala yake
alikwenda Moshi kukata tiketi ya basi la saa sita linalokwenda Dar.
Majira ya
Saa 7:00 mchana, Artha alimpigia simu Angel kumfahamisha juu ya safari
yake na baadaye akawasiliana na mshitakiwa na kwamba mtuhumiwa
alimuagiza akifika Ubungo achukue teksi hadi Grand Hotel ya Magomeni.
Baada ya
kufika hotelini hapo, Artha alipokelewa na mshitakiwa na kwa pamoja
waliingia mapokezi ambapo mtuhumiwa huyo alilipia gharama zote za malazi
ya kijana huyo huku akimhakikishia kufuatilia taratibu za kupata hati
ya kusafiria siku inayofuata.
ANGEL NAYE ATIMKIA DAR
Mwendesha
Mashitaka Chavula aliendelea kuieleza mahakama kuwa, siku mbili baada
ya Artha kufika Dar, Februari 20, Angel alitumiwa shilingi laki moja kwa
mtandao kupitia simu ya dereva teksi.
Katika
fedha hizo, Sh. 40,000 alitumia kama nauli ya teksi kumtoa Masama hadi
Moshi Mjini na zilizosalia, Sh. 60,000 zilitumika kwa nauli ya kwenda
Dar.
Chavula
alidai kuwa Angel alitumia Sh. 18,000 kukata tiketi ya basi na kwamba
mara tu baada ya kufika Dar, alipokelewa na mshitakiwa huyo katika
Hoteli ya Grand.
MCHUNGAJI ATAKA PENZI BILA KINGA
Katika
jambo lililoshtua wengi mahakamani hapo ni pale mwendesha mashitaka huyo
alipoiambia korti kuwa mshitakiwa alitaka penzi kwa Angel.
Alisema
kuwa katika harakati za kufanikisha azma yake ya kufanya mapenzi na
Angel, mchungaji Bamana alikuwa akishinda kutwa katika chumba cha
msichana huyo.
Ilidaiwa kuwa mchungaji huyo alikuwa akimshawishi Angel kwa njia zote kufanya naye mapenzi bila kinga!
Mwendesha
mashitaka huyo alisema kuwa mara zote, Angel alikataa na kumshauri
mchungaji kuwa kama anataka kufanya naye mchezo huo mchafu basi atumie
kinga, kitu ambacho mchungaji huyo hakuwa tayari kukifanya.
Ilielezwa
kuwa baada ya kugonga mwamba kupata penzi, mchungaji aliambulia
kumshikashika na kumbusu mara kwa mara, kitendo kilichomfanya mdogo wake
Angel, Artha aanze kuingiwa na shaka pamoja na kwamba walikuwa
wakitarajia kusaidiwa.
MCHUNGAJI AKANA MASHITAKA
Upande wa
mshitakiwa ulipotakiwa kuwasilisha utetezi wa mashitaka yote mawili,
mshitakiwa akiongozwa na mawakili wawili, Erick Gabriel na Rongino
Myovela pamoja na kukubaliana na maelezo lakini walikana mashitaka yote.
MASHAHIDI
Kutokana
na ugumu wa shitaka hilo, mwendesha mashitaka baada ya kushauriana na
mawakili wa mchungaji, aliiomba mahakama iahirishe zoezi la kusikilizwa
kwa kesi hadi pale upande wa mshitakiwa utakapopeleka mashahidi nane na
vielelezo.
Baada ya
kujiridhisha na maelezo ya upande wa mashitaka na kukubaliana na ombi la
mwendesha mashitaka, Hakimu Mwerinde aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 3,
mwaka huu itakaposikilizwa tena.



