Dada yake msanii Diamond Platnumz, Esma Abdul, amesema wamejiandaa
vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae anatarajiwa kumuoa VJ Penny.
Esma ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, “Tumemkubali sana
wifi yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa
siwezi nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye
ataniingilia kwenye mapenzi yangu.”
Huu ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema
nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini
itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa.
Dada yake Diamond aka wifi yake Penny
Zaidi ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake
imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia
akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan –
Hyundai IX 35.
Mpaka sasa Mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa
Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye
headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma
kama Jokate, Wema Sepetu na wengine.
Chanzo: Millard Ayo