Habarini wana jf, kwa hali ya mambo inayoendelea katika bunge la jamhuri
ya muungano wa Tanzania, ni wazi kuwa wabunge wengi wamepoteza sifa ya
uwakilishi kwa wananchi katika jengo lile la bunge mjini dodoma, wabunge
wengi wameonekana kuwa wasemaji wa serikali na si wa wananchi! Kufuatia
hali hiyo kwa uchunguzi wangu usio rasmi, nimegundua wako baadhi ya
wabunge wachache bado wana moyo wa uzalendo kwa wananchi na taifa lao
kiujumla! Wafuatao ni wabunge watano bora kwa uzalendo na utumishi
uliotukuka kwa wananchi wao waliowatuma bungeni:
1. Mh. Tundu Lissu(chadema)-singida mashariki.
2. Mh. John Mnyika(chadema)- Ubungo.
3. Mh. Deo Filikunjombe(ccm)-Ludewa
4. Mh. Kangi Lugora(ccm)-Mwibara.
5. Mh. Halima mdee(chadema)-kawe!
Pongezi ziende kwa wananchi waliotuchagulia wabunge hao, pia pongeze
ziende kwa waheshimiwa wahusika! Mungu awalinde na kuwapa baraka zake!
Nawasilisha.