Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao. |
Kwa hari isiyokuwa ya kutegemewa kabisa
katika uwanja wa taifa hapo jana mchezaji wa zamani wa klabu ya yanga
ambaye kwa sasa anachezea klabu ya simba Mrisho Ngsa alionekana kubebwa
na Mashabiki waliovalia jezi ya klabu ya yanga yenye maskani yake
Jangwani.
Mrisho ngasa aliwahi kuchezea klabu
hiyo na baadae kuhamia Azam fc ambapo alikaa katika klabu hiyo zaidi ya
miaka mitatu lakini alionekana kubusu jezi ya Yanga wakati akichezea
klabu hiyo ya azam fc katika michuano ya kombe la kagame lakini kabla ya
mechi ya jana kulikuwa na tetesi nyingi zikimuhusisha mchezaji huyo
kurejea katika klabu yake ya zamani yanga .
Habari ambazo zilizua minong'ono kadhaa
katika vyombo vya habari na majibizano ya baadhi ya viongozi wa timu
zote mbili .kama ilivyokuwa siku ya kubusu jezi ya yanga ilionekana ni
mwiba mchungu kwa Azam ambao hawakufurahi kabisa kitendo cha mchezaji
huyo kubusu jezi hiyo ilighari akiwa amevalia jezi Azam fc.
Lakini jana mara baada ya mpira
kumalizika mchezaji huyo alionekana kubebwa na Mashabiki waliovalia jezi
ya mabingwa wa ligi ya soka ya kandanda Tanzania bara Dar es salaam
young afrika
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao. |
Hili sio jambo Rahisi katika klabu za
mpira wa tanzania hasa kwa timu ambazo zinazidi kushika umaarufu katika
soka ya afrika Mrisho Ngasa anaweza au mashabiki hawa waliombeba
wanaweza kuona wamefanya jambo dogo au wanajua kabisa Tukio
wanalolifanya sasa' linaweza kuzua mijadara mbalimbali katika vyombo vya
habari hasa ukizingatia ni timu mbili pinzani
kwa upande mwingine ni tofauti sana na
nchi zilizo endelea kuona tukio kama hili wapo wachezaji duniani ambao
wanaweza kuhamia timu pinzani lakini wakaweka heshima na kutokuonyesha
dalili za aina yoyote kama kuna mahusiano ya wao kuhamia timu pinzani.
kwa umma wa watanzania na mashabiki
wengi wanajua fika kuwa Ngasa bado yupo simba bila kuona nyaraka za
utiaji saini kwani isingekuwa hivyo tff isingemrughusu kuchezea simba
lakini tutazame kwa sasa picha hii inayoonekana sasa ina maana gani kwa
ngasa mwenyewe ,mashabiki wa timu zote mbili pamoja na viongozi wa timu
zote ,Ngasa anaoneakana Mwingi wa tabasamu sana usoni lakini ataaendelea
kutasabasamu mpaka mwisho Mrisho ngasa aliondoka yanga baada ya
kuoneakana kwenda rwanda kujaribu kuchezea APR kocha mkuu wa yanga
wakati huo alikuwa Dusan Kondic ambaye kwa mujibu wa mwenyekiti wa
yanga wakati huo imani madega alisema kocha ameona ni kheri wamuuze huyu alikuwa ni mkufunzi wa kigeni
na wakati alipokuwa Azam fc alikuwa
chini ya Sterwart Jonh hall ambaye hakulalamika sana kwa mchezaji huyo
kuperekwa simba japokuwa ilisemekana kuwa alikwenda kwa mkopo huku
baadaae ikidaiwa mchezaji huyo ameingia kandarasi ya muda mrefu hapa
nikutaka kukuonyesha farsafa za makocha wa kigeni zilivyo jambo rahisi
zaidi ni kwamba hatutashangaa sana kuona Mfaransa huyo wa simba Patrick
Liewing akiridhia Ngasa kuondoka .
kama atafanikiwa kurejea Yanga je ni upi utakuwa mustakbali wa maisha
ya kisoka ya mchezji huyu wa simba kwa sasa pengine hata kama ana
mapenzi na Yanga kulikuwa na haja gani ya kuonyesha dhahiri kiasi kile
hasa katika mechi ambayo unacheza timu pinzania na unayopipenda au ndio
kujiwekea maandalizi ya kuondoka au kutaka ufukuzwe urejee timu yako ya
zamani .
kwa hakika wapo wachezaji wengi wenye mapenzi na timu zao binafsi kiasi kwamba hata kama akicheza nayo huendelea kuifunga
kama kawaida lakini je ni kweli kuwa ngasa hakuataka kuifunga yaga
jana tena kwa penati ambayo alifanyiwa faulo yeye mwenyewe kwa sasa Tanzania inatakiwa kutizama mafuzno ya kweli ya mpira wa kulipwa kwani kimaitafa wanaposema mpira wa kulipwa hawazungumzii fedha." hata tabia kiwanjani na jinsi unavyoewa kuishi na wachezaji wengine na mashabiki wa timu tofauti na wewe ,
JE NINI MAISHA YA BAADAE YA MRISHO NGASA WA SIMBA