Familia
ya rapper Hov na Queen Bey inategemea kumpa binti yao wa kwanza Blue
Ivy mdogo wake. Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika Beyonce ana ujauzito wa
pili.
Taarifa za ujauzito wa pili wa
Beyonce mwenye miaka 31 zimethibitishwa jana May 17 na vyanzo tofauti
na kuripotiwa na vyombo vingi vya habari ikiwa ni siku chache toka
acancel show yake ya Mrs Cartter World tour huko Antwerp, Belgium
kutokana na upungufu wa maji mwilini na uchovu (dehydration and
exhaustion).
Tetesi za ujauzito wa pili wa
Beyonce zimeunganishwa na maelezo aliyoitoa Bey mwenyewe katika
mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha ABC, “napenda kupata watoto
zaidi, nadhani binti yangu anahitaji kupata company.”
Kwa kumbukumbu zetu, Jay na
Beyonce ambao ni wa kwanza kuwa ‘billion dollar couple’ katika muziki
imekuwa na kawaida ya kufanya mambo yao kwa usiri mkubwa hasa katika
kipindi ambacho wanakuwa hawajaamua kuzifanya zijulikane.
Itakumbukwa wakati wanafunga
ndoa iliwachukua muda mpaka watu kujua walifunga ndoa ya siri. Pia
wakati wa siku za mwanzo za ujauzito wa Blue Ivy hawakuweza kuthibitika
mapema kuwa Queen Bey alikuwa mjamzito, na baada ya Blue Ivy kuzaliwa
haikuwa kazi rahisi kwa camera za mapaparazi kukiona kichanga chao mpaka
muda ulipopita.