Chanzo
chetu makini cha mtandao huu wa kingjofa.blogspot.com kilifanikiwa
kuzungumza na
mratibu wa mashindano hayo Mkurugenzi
wa kampuni ya New Vision Plan inayohusika na kazi za kuandaa mashindano
ya ulimbwende, Moses Komba alisema kuwa jumla ya walibwende wapatao 19
wapo tayari kuchuana vikali maana kila mlimbwende anavigezo vya kushinda
kwenye kinyang'anyiro hicho cha kumsaka Miss Moshi. Warembo hao
waliofanyia mazoezi katika ukumbi wa aventure na leo hii ndio siku ya
kutimua vumbi katika ukumbi huo. Na mpaka sasa kila kitu kinakwenda
sawa.
Katika shindano hilo ambalo wadhamini wukuu ni Redds na kampuni ya Panone and Company Limited na wadhamini wengine ni kama Baba G na Zoom Net Printers ambapo kwa upande wa burudani atakuwepo msanii mkongwe wa kizazi kipya Dully Sykes akisindikizwa na wasanii wengine kutoka Moshi.. Moses Komba
alisema kwa taratibu za kuingia Kwenye ukumbi wa Aventure Africa utakua
kama ifuatavyo kwa viti vya dhahabu vitakuwa sh. 50,000, viti vya
Silver vitakuwa ni sh. 30,000 na
viti vya kawaida ni sh. 15,000.