ICHEKI VIDEO HII P- FUNK AKIWACHANA CLOUDS FM AELEZA JINSI MAREHEMU MAGWEA ALIVYOGEUZWA NG'OMBE WA MAZIWA
Kwa
mara nyingine tena P-Funk amezungumzia sababu anazodhani zilipelekea
marehemu Ngwea kujiingiza kwenye madawa.
Producer huyo ameichana CloudsFM kwa kile anachokiona kama unyanyasaji
kwa wasanii, na kwamba dhuluma za Clouds Fm ni moja wapo ya vitu
vilivyosababisha maisha ya Ngwear yawe na muelekeo mbaya.
“Ngwair alikua kama ng’ombe wenu; mnamkamua tu maziwa.” P funk
Akizungumzia kuhusu kuikataza Clouds FM kupiga nyimbo za Bongo Records
zikiwemo wa Ngwea, P-Funk amesema:
“Niko kwenye harakati za kuandaa barua ili nistopishe nyimbo zangu zote
za Bongo Records, zisipigwe Clouds Fm.
Sababu kubwa ni uonevu wa haki miliki. Eti mnajiita number one radio
station??. Mnajidaganya .Kisaikolojia wasanii wote mmewateka.
Wote wanaona “bila kupeleka nyimbo zao Clouds hawatafanikiwa.”Mimi cha
kwanza nataka kuonyesha mfumo mwingine kwamba bila nyinyi tutaweza. Cha
pili mnaingiza hela sana ya wadhamini lakini hamui-distribute kwa
wanaohusika...
"Mfumo wa kupeleka nyimbo Clouds nilianzisha mimi . Hivyo nitakua wa
kwanza kujitoa na kuanzisha mfumo mwingine.””