FAMILIA
 ya mme, mke na mtoto wamenusurika mkoani hapa, baada ya gari aina ya 
Noah, kuacha njia na kuwafuata chumbani wakiwa wamelala usiku wa manane.
Tukio
  hilo la aina yake, limetokea saa nane usiku wa kuamkia leo, kwenye 
chumba cha familia ya Adam Gau kilichopo katika nyumba ya Eliasi 
Chebuse, iliyopo kiasi cha mita tano kutoka barabara ya Jamhuri, mjini 
Dodoma.
Akizungumzia
 tukio hilo leo asubuhi, Chiku ambaye ni mke wa Gau alisema, akiwa 
amelala na mumewe na mtoto wao mwenye umri wa miaka minne, Muumin Adam, 
walisikia kishindo kikubwa kilichoambatana na sehemu kubwa ya ukuta wa 
chumba kuporomokea ndani. Pichani askari ambvaye pia ni mkazi wa nyumba 
hiyo akionyesha madhara yaliyotokana na chumba kugongwa na gari. Kushoto
 ni Mama Gau






