Katika tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV 
kiliandaa mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala 
mbalimbali ya kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika 
wasemaji wakuu wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya 
Siasa wakianza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu 
Abdulrahaman Kinana naKatibu Mkuu wa CDM Ndugu Slaa.
Kutokana na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri
 kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa 
na majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa 
Itikadi na Uenezi CCM,ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo
 wa viongozi wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na 
mustakabali wan chi yetu.
Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo, 
Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha 
Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli 
hiyo, Dr Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa 
sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake.
Hata busara zilipotumika za kumsihi apungumze munkari na kumtaka 
kuangalia umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa watanzania, 
bado Slaa aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV.
Baada ya tahamaki hiyo, mijadala ya pembeni ya mashuhuda wa tukio hilo 
walieleza kuwa kimsingi Slaa anamuogopa Nape katika mijadala ya kisiasa,
 nahii ni kutokana na uwezo wa Nape katika kujenga hoja na kuzilinda na 
kuzitetea hoja hizo...
Tukio hilo linadhihirisha kukosa uvumilivu wa kisiasa (lack of political
 tolerance) ambako viongozi wa CDM hasa Slaa wanao..... Hii ni kwa 
sababu Nape alimtaka aeleze ni kusemwa vibaya kupi ambako yeye Slaa 
anakumaanisha na akashindwa kubainisha.....
Hali hiyo pia imeonesha taswira ya political immaturity kuwa viongozi wa aina hii hawajakomaa ...
Pia, tukio hilo linaweka wazi kuwa CDM hawako tayari kuyazungumzia ana 
kwa ana matatizo yaliyotokana na Siasa mbovu za matusi....
Tabia hii ya kukwepa kuyashughulikia makosa ya kisiasa kutalileta Taifa 
letu madhara makubwa sana. ...kukataa kulikubali tatizo tulilonao la 
siasa mbofu zenye kuhamasisha chuki, utengano, udini, ukabila na hata 
kuendesha matukio ya kudhuru watu na mauaji ni makosa.




