Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Omar Kinana, kupitia kwa wanasheria
wa LAW OFFICES OF ERIC S. NG'MARYO wa Moshi amemuandikia Mbunge wa
Iringa Ndugu Peter Msigwa agizo la kumtaka amuombe radhi kwa matamshi
ambayo kinana anadai ni ya uongo kwamba,
HII NI SEHEMU YA BARUA HIYO:
"Nakuandikia kwa maagizo niliyopewa na mteja wangu, Ndugu Abdulrahman
Kinana, kufuatia matamshi yako ya uwongo ambayo yamemkashifu,
kumfedhehesha na kumshushia hadhi, Matamshi hayo uliyoyatoa mchana wa
tarehe 21 April, 2013 katika mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika
kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani, Wilaya ya Nyamagana, jijini
Mwanza.
Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wengi. Pamoja na watu hao walikuwepo
pia waandishi wa habari, wakiwepo wanahabari wa magazeti, radio
televisioni. Habari zenye Maneno yako ya Kashfa zimeenea nchi nzima na
duniani kote kwa njia ya habari elektoniki, ikiwepo mitandao ya
kijamii.
Habari hizo zinaendelea kusomwa hadi sasa, na zitabaki kuwa kumbukumbu
ya kudumu katika intaneti na kwenye hifadhi nyingine za habari"
"Katika Mkutano huo, ulisikika ukisema maneno mengi ya Kashfa kwa mteja
wangu, yakiwemo haya yafuatayo: Kinana (na naomba waandishi w habari
mnisikie na nyie usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita
barabarani na kuwaambia watanzania waiamini ccm.
Kinana mikono yake si misafi hata kwenye NASACO, Shirika la Meli
Tanzania, kuna harufu ya ufisadi ndani yake, ajibu hapa... Kinana Meli
zake ndio zinahusika kubeba mapembe nchi hii, hajajibu hoja hizo! kwa
siku katika nchi hii tembo sitini na saba wanauwawa...
Hao ndio wanaokifadhili Chama cha Mapinduzi wakina Kinana halafu
wanakuja eti kuwashawishi watanzania muwasikilize na kwamba Chama cha
Mapinduzi eti ni kizuri.
Halafu leo tukikaa ndani ya Bunge tunapojaribu kuwatetea wananchi
tumeacha majimbo yetu, Haya mambo ninayaongea ni hatari kwa sababu haya
yote ni majangiri ni organized crime ni mtandao wa kimataifa uko duniani
kote. unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea.."
Katika barua hiyo, mwanasheria huyo amemtaka Msigwa amuombe msamaha
yaishe au la atamvuruta mahakamani, tena kwa vitisho .Nainukuu para ya
mwisho :
"Nakuangaliza na kukutahadharisha kwamba iwapo hutatimiza matakwa ya
Mteja wangu kama yalivyoainishwa kwenye barua hii, basi kesi itakayokuja
dhidi yako itakuwa na madai makubwa na mengi kuliko yale yaliyotajwa
humu, na unaweza kubebeshwa mzigo wa uharibifu, hasara na madhara
uliyomsababishia Mteja wangu, pamoja na gharama za kesi nzima, ambazo
zote zinaweza kufikia mamilioni ya Shilingi za Kitanzania"
Kuna para kumi na mbili za barua hiyo ambazo zinapatikana ukurasa wa 25 wa gazeti la mwananchi.
credit- mpekuzi