Katherine B. O'Connor akifanya dhihaka zake.
Mwanafunzi mmoja wa kike wa Chuo
Kikuu cha Carnegie Mellon ameshitakiwa Ijumaa kwa hali ya uvunjaji
heshima na polisi wa kampasi baada ya Askofu Katoliki kulalamika kuhusu
kutembea kwake hadharani akiwa uchi kuanzia kiunoni kwenda chini huku
kavalia kama Papa.
Mwanafunzi
mmoja wa kiume ambaye alikuwa uchi pia ameshitakiwa, lakini
haikufahamika mara moja alichokuwa akifanya wakati wa gwaride la sanaa
ya uchoraji la majira ya bamvua ya Shule ya Pittsburgh mwezi uliopita. Rais
wa Chuo hicho, Jared Cohon alisema Ijumaa iliyopita kwamba mashitaka
hayo madogo yalikuwa yamefunguliwa huko Allegheny County dhidi ya
wanafunzi hao wawili na kwamba shule hiyo haitachukua hatua zozote zaidi
za kinidhamu. Alisema shule hiyo imebariki kujieleza kisanii lakini kujianika uchi hadharani ni kinyume cha sheria. "Kuna
ushindani wa thamani katika suala hapa: Carnegie Mellon inakusudia kuwa
sehemu ambako mawazo yanaweza kuwasilishwa na kujadiliwa kwa uwazi,
lakini pia ambapo watu wa historia zote, dini, na imani kujisikia
wanakaribishwa na kupewa msaada," alisema Cohon. Askofu David Zubik
wa Dayosisi Katoliki ya Pittsburgh alilalamika baada ya gwaride hilo
Aprili 18, ambapo mwanafunzi huyo wa kike - huku nywele zake za sehemu
za siri zikiwa zimenyolewa kwa alama ya msalaba - alirusha kondomu kwa
watazamaji. Cohon aliomba radhi wiki iliyopita kwa onesho hilo. Chuo
hicho hakikuwataja wanafunzi hao wawili. Rekodi za mahakama zinaonesha
wanafunzi hao Katherine B. O'Connor, miaka 19, kutoka Pittsburgh, na
Robb S. Godshaw, miaka 22, kutoka Wilmette, Illinois, walishitakiwa na
polisi wa kampasi kwa tukio la uvunjaji heshima. Hakuna mwanasheria
aliyekuwa amejitokeza kumtetea yeyote. Si O'Connor wala Godshaw aliyejibu ombi la kutoa maoni yoyote kuhusiana na suala hilo. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa kwa mara ya kwanza Juni 10, mwaka huu. Zubik alisema katika taarifa Ijumaa kwamba Chuo Kikuu hicho kinalichukulia 'tukio hili lisilotarajiwa' kwa uzito wa kipekee. |