Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 wakiwa katika Picha ya Pamoja.
Baada
ya shamlashamla na mapokezi makubwa ya Miss Utalii Tanzania walipo
ingia Mkoani Tanga na kupokelewa na umati mkubwa wa watu, warembo hao
wapo kambini tayari kwa maandalizi ya Fainali hizo.
Fainali
za Taifa Miss Utalii Tanzania zitafanyika Tarehe 19.05.2013 Mkoani
Tanga ambapo warembo zaidi ya 30 watapanda Jukwaani kuwania Taji la
Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013 ndani ya Mkwakwani.
Sambamba
na Fainali hizo za Miss Utalii , kutakuwa na Burudani ya Kukata na
shoka ambayo itasindikizwa na Bendi kongwe ya Muziki Msondo Ngoma kutoka
Dar es salaam, Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao, Majuto Arts
Group, Mdumange, vikundi vya ngoma na Sarakasi.
Fainali
za Taifa zitaanza kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 jioni Ambapo
viingilio kwa watoto itakuwa 2,000 na wakubwa 5,000 Baada ya hapo
kuanzia saa 1 usiku hadi Majogoo viti Maalum itakuwa ni 20,000 na
kawaida itakuwa 10,000
Mpaka
sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel
na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini
,wanajiandaa vizuri kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki
ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
Washindi
wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano
mbalimbali ya Dunia na nchi yatakako fanyika katika
mabano International Miss Tourism World (Marekani), Miss Tourism United
Nation (Mexico), Miss Heritage World (Tunasubiri Taarifa), Miss
Tourism University World(Tanzania), Miss Globe International (Uturuki),
Miss Tourism World ( Equatorial Guinea ), Miss Freedom Of The World (
Kosovo) , na Miss Tourism United Nation (Nigeria) n.k
Wakati
huohuo, katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya Fainali za taifa, za
mashindano hayo ambapo mkoa wa Tanga unakuwa wenyeji kwa mara ya kwanza
yanafanyika kwa ubora na hayakwami, kamati ya maandalizi ya kimkoa
umeundwa ambayo mwenyekiti wake ni Peter Semfuko Afisa Utamaduni wa Jiji
la Tanga.
Miss
Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na
kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World
2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism Model Of The World 2008-Personality, Miss Africa 2006 – 1ST Runner Up n.k