News
is that actress Kajala Masanja anatarajia kucheza katika filamu ambayo
itaelezea maisha yake halisi ya kesi yake iliyokuwa ikimkabili. filamu
hiyo itaelezea tangu mwazo wa issue hilo, mahakamani, segerea mpaka
anatoka baada ya Wema Sepetu kumtolea faini ya sh. millioni 13. Kajala
mwenyewe amesema ni kweli na kwasasa story na script ndiyo vinafanyiwa
kazi. Hata hivyo wadau wanaweza kuwa na hamu ya kuiona filamu hiyo kama
kweli itafanikiwa kuonyesha mazingira halisi ya mahakamani na segerea
kama ilivyokuwa kwa mwigizaji huyo kabla ya kuwa uraiani ikichukuliwa
kwamba bado ni shida sana kupata location katika taasisi za serikali
hasa huko segerea ambako Kajala mwenyewe aliwahi kusema kuna mambo ya
kuhuzunisha sana.
Kwasasa
inadaiwa Kajala anafanya filamu ya Princess Sasha chini ya Wema Sepetu
huku tayari baadhi ya watu wakisema Kajala ana haraka sana pengine
ameburuzwa na watu kuhusu kucheza story ya kesi yake kwakuwa bado mumewe
yupo jela hajatoka lakini tayari yeye amepanga yake huku uraiani.
Shabiki mmoja amesema " i think Kajala bado hajashauriwa vizuri kwa time
hii kucheza maisha yake halisi hata miezi 2 bado kuisha". mashabiki
wake wengine wamesema ni poa tu apige kazi " Kajala Nakuaminia Pamoja Sana Kazi Njema" amesema shabiki yake mmoja.