Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, May 10, 2013

BABA YAKE INIESTA AMSHAMBULIA JOSE MOURINHO

José Antonio Iniesta ameamua kumtolea uvivu Kocha Mkuu wa Real Madrid, José Mourinho.

Jose, baba wa kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta amesema kocha huyo Mreno hana nidhamu na ameharibu mpira wa Hispania hasa kwa kumshambulia mwanaye.

"Nimechukizwa na Mourinho kumshambulia Andres kwa kuwa hakuwa na kosa kumzungumzia Iker (Casillas) kwa kuwa wana uhusiano mzuri.

“Wote wanacheza pamoja timu ya taifa, wamefanya kazi vizuri katika timu hiyo. Sasa tatizo lilikuwa ni lipi kumzungumzia? Kweli si mtu mzuri na hana heshima,” alisema Jose wakati akizungumza na redio Marca.

Hivi karibuni, Iniesta alisema Casillas ana nafasi ya kuendelea kuichezea Madrid na anaona si sahihi akiendelea kubaki benchi.

Hali hiyo ilionyesha kumuudhi Mourinho ambaye alimshambulia Iniesta kwamba hapaswi kuingilia mambo ya Madrid na aachane na kuwa mdomo mkubwa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...