Ushindi huu umetokana na uongozi bora, uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya klabu na kufikia malengo.
Mwenyekiti wetu ametujengea dhana ya kuwa na imani ndani ya uongozi, wanachama na wachezaji wetu.
Hivyo basi na sisi kama wazee wa Klabu tunayo imani na viongozi na
wachezaji wetu na tunaahidi kuwa mchezo wetu wa tarehe 18 Mei 2013 kati yetu na Simba lazima tushinde ili tusherehekee Ubingwa wetu kwa furaha, shangwe na nderemo.
“YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”
K.n.y: YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB na MWENYEKITI WA WAZEE
YANGA ALHAJ JABIRI M. KATUNDU