Kustaafu ndio habari iliyoshika hatamu nchini Uingereza hiv sasa - wiki
moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo
hii mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa
England DAVID BECKHAM ametangaza kutundika daluga.
Beckham, 38, ameisadia Paris Saint-Germain kubeba kombe la Ligue 1 kwa mara ya kwanza ndani miaka 19 mwishoni mwa wiki hii.
Pamoja na kupewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa,
mkongwe huyo atastaafu baada ya mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huu.
Alisema: “Shukrani sana kwa PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa
hapa lakini sasa nadhani ni muda sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka
la kiwango cha juu”
Becks alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid.
Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007
pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan
wakati akiwa kwenye Major League Soccer.