Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, January 3, 2014

NHIF yatatizwa na wanachama wadanganyifu


Ukiukwaji wa utaratibu wa kujumuisha wategemezi  wanaostahili kupata huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), unatishia uhai wa mfuko huo ambao hadi sasa umeishafikisha mahakamani kesi zaidi ya 18 katika mahakama 
 

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Hamisi Mdee alisema kuna udanganyifu mkubwa ambao unafanyika katika uandikishaji wa wategemezi wanaostahili huduma za matibabu.

Alisema udanganyifu mkubwa unafanywa na baadhi ya wanachama wa mfuko huo ambao wanauza nafasi za wategemezi wao kwa watu wenya mahitaji makubwa ya matibabu ili kujipatia fedha kinyume cha sheria hususan wale wa magonjwa ya figo na saratani.

Mdee alisema mgonjwa anayehitaji kusafishwa figo mathalani husafishwa mara tatu kwa wiki na inagharimu sh300,000 kwa mara moja kiwango ambacho ni sawa na sh900,000 na upande wa saratani kipimo cha ugonjwa huo (Chemotheraphy) ni  sh1.3 milioni hadi 4 na dozi nzima ni sh24 milioni.

“Watu wanauza majina ya wategemezi wao kwa watu wengine jambo ambalo linautia mfuko hasara na kutishia kuwepo kwake” Mdee alisema na kuongeza kuwa kutokana na hali hiyo mpango huo ni endelevu hivyo hugharimu mfuko fedha nyingi na mbaya zaidi ni kwa watu ambao si walengwa.

Alisema kutokana na kubainika kwa ulgahai na hujuma za namna iyo mfumo hivi sasa umeweka utaratibu wa usajili wa wategemezi wanaolengwa na mfumo ambao ni pamoja na mwenza halali wa mwanachama mchangiaji.

Wengine ni watoto wa kuzaa au kuasili wa mwanachama mchangiaji, wazazi wa mwanachama na au wazazi wa mwenzi wake na kulingana na utaratibu huo kuanzia hivi sasa huduma za matibabu zitatolewa kwa wale tu wenye vitambulisho na sio vinginevyo kulingana na utaratibu wa sasa.

Siku za karibuni kumekuwa na matukio mengi ya watu kukamatwa wakitumia vitambulisho vya watu wengine ili kupata matibabu ya maradhi mbalimbali na maeneo mengine wamekuwa wakipata huduma hizo bila kubainika jambo ambalo linaugharimu mfuko.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...