Mtangazaji wa Radio Nuru Fm Emmanuel Mwansasu akifuatilia show ya Mtikisiko 2013
ONYESHO kubwa la kufunga mwaka la
Mtikisiko na radio Ebony Fm 2013 Iringa limevunja rekodi ya umati wa
watu kuingia katika uwanja wa Samora toka show kama hizo zilipoanza
katika uwanja huo kwa zaidi ya miaka minne sasa .
Mbali ya Show hiyo kupata umati
mkubwa wa watu pia idadi kubwa ya wasanii walioletwa katika show
hiyo walijikuta si lolote mbele ya msanii Madee kupitia wimbo wake
wa Nani kamwaga pombe yangu baada ya shabiki wake ambae alikuwa
amelewa chakali kumvamia msanii huyo jukwaani wakati akiimba wimbo
huo wa nani kamwaga pombe yangu huku mlevi huyo akiitikia ni mimi
nimemwaga pombe yako na nipo tayari kukumwagia na hii.
Mlevi huyo ambae alikuwa na chupa ya
pombe mkononi alianza kumkumbatia msanii huyo huku akiangua kilio
kiasi cha askari na timu ya ulinzi uwanjani hapo kupanda jukwaani na
kumng'amua katika mwili wa msanii Madee
Wakati msanii Madee akivamiwa jukwaani
na mlevi bado watu wa ulinzi walijikuta katika wakati mgumu
kumthibiti msanii huyo ambae alionyesha kupendwa zaidi na mashabiki
uwanjani hapo.
Kama haitoshi msanii Shilole pia
aliwapa wakati mgumu polisi baada ya kuruka jukwaani na kuwafuata
mashabiki hali iliyozua hofu zaidi uwanjani hapo kutokana na kundi la
vijana waliopangwa na mzuka wa nyimbo za msanii huyo kutaka
kumng'ang'ania kiuno kwa kila mmoja akitaka kushika mwili wa msanii
huyo kwa kucheza nae.
Kutokana na polisi kufanikiwa
kumthibiti msanii huyo na kumrudisha jukwaani mashabiki walionyesha
kuchukizwa kutokana na polisi kumtoa eneo hilo la mashabiki kiusalama
na kumrejesha jukwaani na hivyo kuanza kurusha chupa za maji
wakitaka kumwachia huru msanii huyo awazungushie mauno.
Wasanii wengine waliopagawisha ni
pamoja na msanii baba Revo ,msanii Squza, msani Nyamidela kutoka
Iringa ,msanii Jan Kihaga wa Kihesa Iringa ambao walionyesha kuvutia
wengi katika uwanja huo wa Samora mjini Iringa
|