Mlimbwende Joy Kalemera akipungia mashabiki baada ya kushinda
mashindano ya Miss Tanzania USA Pageant yaliyofanyika usiku wa Jumamosi
Novemba 30, 2013 kwenye ukumbi wa Hollywood Ballroom uliopo Silver
Spring , Maryland na Mhe. Balozi Liberata Mulamula ndiye aliyekua mgeni
rasmi. Joy Kalemera alipohojiwa na Vijimambo alikua na haya ya kusema.
Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalamera akipewa maua na
aliyekua Miss District of Columbia baada ya kutangazwa mshindi kwenye
Miss Tanzania USA Pageant ambapo mashindano haya ya kumtafuta Miss
Tanzania USA Pageant ndiyo ya kwanza kufanyika kwenye ardhi ya
Marekani.
Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera akiwa mwenye furaha baada ya kutangazwa mshinidi wa Miss Tanzania USA Pageant.
Balozi wa Tnzania nchini Marekani na Mexico akimvisha taji Joy Kalemera baada ya kutangazwa mshindi wa Miss Tanzania Pageant
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa mwenye furaha baada ya shindano
hili kufana sana na kuandika historia iliyobeba ukurasa mpya wa
kutangaza Tanzania kwenye mashindano haya ya Miss Afrika USA Pageant
ambayo Tanzania ilikua na mshiriki wa kwanza mwaka huu ambae ushiriki
wake haukupitia ngazi hii.
Joy Kalemera akipongezwa na washiriki wenzake waliokua nae kwenye kinyang'anyiro hiki kilichoanzia miezi miwili iliyopita.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye picha ya pamoja na
mshindi wa kwanza katika historia ya Miss Tanzania USA Pageant Joy
Kalemera kulia ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant
Ma Winny Casey.
Joy Kalemera katika picha ya pamoja na majaji pamoja na mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant, Lady Kate (kulia)
Kutoka kushoto ni Faith Kashaa kutoka Alabama ambaye ndiye mshindi
wa tatu, Doreen Rumaya kutoka Pennsylvania mshindi wa pili, Joy Kalemera
kutoka New Jersey Miss Tanzania USA Pageant, Julia Nyerere mshindi wa
Tano na Namala Elias mshindi wa nne wakiwa kwenye picha ya pamoja
Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na washiriki wenzake.