Lady Jaydee (kulia) akiwa na Prof. Jay (kushoto) pamoja na Gadna (kwa nyuma) wakiwa wanatoka mahakamani leo
Lady Jayde akiwa anatoka nje ya mahakama
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa
kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi
ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi
hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa
kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili
anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi
wake.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama
Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo
kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi
hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na
Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi
huo.
Kwa
mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa
mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi
huo kupitia blogu yake.





