Pia ina smart content, una create account na kupata applications kibao, pia ni tv ambayo unaweza ku-update yani kama Samsung wakileta teknolojia nyingine kwenye Tv hutatakiwa kununua Tv nyingine bali unatakiwa kununua kadi na ku-update hiyo teknolojia mpya.
Tv ya bei ndogo kuliko zote kwa samsung sasa hivi ni inch 19 inayouzwa laki nne na nusu ambapo Tv zinazonunuliwa na Watanzania wengi ni za inch 32, 26, 40, na 46 ambayo ni smart TV unayoweza kuitumia pia kwa kutumia Internet.

Hii
ndio TV kubwa kuliko zote za Samsung ambayo ina inch 75, yani bei yake
ya milioni 24 ni pesa ambayo kama una kipato cha shilingi elfu 30 kwa
siku, kuweza kuinunua inabidi usile wala kunywa au kufanya chochote
kwenye hiyo elfu 30, uikusanye kwa siku mia nane (800)





