MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rachel Haule ‘Recho’ alijikuta akichezea
kibao cha ukweli na kusababisha aangue kilio wakati alipokuwa akirekodi
sinema.shuhuda wa tukio hilo lililotokea maeneo ya Mwenge, jijini Dar
alisema msanii huyo alikuwa katika kurekodi moja ya vipande vya sinema
yake mpya lakini kutokana na matakwa ya filamu hiyo kuonesha hisia za
kulia, ilibidi Baba Haji amshushie kofi fastafasta.
“Siku hiyo sikuwa kwenye ‘mudi’ sababu
kuna mambo yalinichanganya, nilishindwa kuvuta hisia za kulia ndipo
niliposhtukia kofi la Baba Haji na machozi yalinitoka yenyewe, hii kazi
yetu hii we acha tu,” alisema Recho.