Mashine za NSSF ALL MEDIA GROUP, waheshimiwa wabunge walilala katika dimba lao la nyumbani
NSSF
VS WABUNGE kazi ilikuwa si mchezo, ulipigwa mpira mkubwa sana, lakini
waheshimiwa walibamizwa kwa mara ya kwanza katika uwanja wao wa nyumbani
wa Jamhuri mkoani Dodoma
Na Mwandishi wetu
TIMU
inayoundwa na wachezaji kutoka vyombo vya habari mbali mbali
vilivyoshiriki katika michuano ya NSSF “NSSF Media All Stars” imevunja
mwiko wa timu ya Bunge FC ya kutofungwa kwa miaka tisa baada ya kuichapa
kwa bao 1-0.
Katika
mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri na kuhudhuliwa na
watazamaji wengi katika historia ya uwanja wa Jamhuri, ulikuwa mkali na
wa kusisimua na timu zote zilishambuliana kwa zamu.
NSSF
All Media ilianza mchezo huo kwa kasi kufanya mashambulizi makali
katika dakika 10 za kwanza. Julius Kihampa alikosa bao la wazi katika
dakika ya pili baada ya pasi safi kutoka kwa Mbozi Katala ambaye
alishirikiana vyema na Maulid Kitenge, Wilbert Molandi na Emmanuel
China.
Dakika
ya saba, shuti la faulo iliyopigwa na nahodha wa timu hiyo, Majuto
“Ronaldo” Omary iligonga mwamba baada ya kumshinda kipa wa Bunge FC Idd
Azzan ambaye hakuweza kufanya lolote.
NSSF
All Media ilisheherekea bao lake pekee katika dakika ya tisa kwa kichwa
kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Majuto ambaye aliwatoka walinzi
wawili kutoka upande wa kulia na kupiga krisi safi.
Bunge
FC ilijikuta ikiutafuta mpira kwa tochi muda mwingi, ilishindwa kufanya
mashambulizi ya kina karibu dakika 70 na kuifanya NSSF All Media Stars
iliyokuwa chini ya kocha wake, mchezaji wa zamani wa mabingwa wa soka
nchini Yanga, Sanifu Lazaro ilitawala muda mwingi.
Baada
ya goli hilo Bunge FC walijitahidi kushambulia lakini ngome ya NSSF
Media Cup Stars FC chini ya kipa Said Ambua ilikuwa imara kuokoa hatari
zote langoni.
Katika
mechi ya wanawake, Bunge Quuens iliyokuwa ikiongozwa na Halima Mdee
(GK) na Esta Bulaya (WD) ilitoka kifua mbele kwa magoli 31 kwa 18 ya
NSSF Media Cup Stars Queens.
Katika
mechi hiyo iliyoshuhudiwa na mawaziri mbalimbali pamoja na huku mgeni
rasmi akiwa pamoja na Naibu Spika wa Bunge. Bunge Queens ilikuwa
ikiongoza kwa magoli 17-10.
Magoli ya NSSF Media Cup Stars Queens yalifungwa na Lulu Habib na Imani Makongoro (GS) aliyemtoa jasho halima Mdee (GK).
Baada
ya mechi hiyo Naibu Spika, Job Ndugai alizipongeza timu za kombaini za
NSSF hasa ya soka ambayo imeweka rekodi mpya kwa kuwafunga wabunge
kwenye uwanja wao.
“
Mmeonyesha uwezo mzuri lakini pia mmeonyesha kweli nyie ni wachezaji
makini kwani mara kwa mara wabunge hawafungwi hapa Dodoma lakini nyinyi
mmekuwa wa kwanza hongereni sana,” alisema Ndungai ambaye ndiye
alikabidhi vikombe kwa washindi kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa
NSSF, DK Ramadhan Dau.