Kamati ya msiba ya mwanamuziki Albert
Mangwea, imeleta taarifa kwamba mwili wa Ndugu yetu Albert Mangwea
hautoweza kufika siku ya jumapili ya tarehe 2/ 06/2013 kama ilivyo
taarifa hapo awali, hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo
wetu.
Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili
kutoka kwa wenzetu/wawakilishi wetu waliopo nchini Afrika Kusini, mara
tutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba radhi watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza tushirikiane na uvumilivu kwa hili.