Baada
ya Rick Ross kupigwa chini na Reebook, sasa ni zamu ya Tunechi. Lil’
Wayne amepoteza mchongo wake kama msemaji wa kinywaji cha Mountain Dew
kufuatia mashairi kwenye wimbo wake Karate Chop.Lil’
Wayne ambaye amekuwa akitumiwa kwenye matangazo ya Mountain Dew tangu
mwaka 2012, ameikasirisha familia ya Emmitt Till kwenye wimbo “Karate
Chop” ambapo Weezy anasikika akisema, “Pop a lot of pain pills, ’bout to
put rims on my skateboard wheels … beat that p***y up like Emmett
Till.”
Emmett Louis
Till alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyeuawa huko
Mississippi mwaka 1955 akiwa na miaka 14 baada ya kumtongoza msichana wa
kizungu.
Licha ya kutuma barua ya kuomba radhi kwenye familia hiyo, ilikataliwa na ndugu zake pamoja umma kumkosoa vikali Lil Wayne.
Japo kampuni ya Pepsi haijatoa
maelezo zaidi, hatua hiyo ilitangazwa na msemaji wa Lil Wayne Sarah
Cunningham, aliyesema kuwa ni kutokana na kupishana kiubunifu