Serikali
ya Tanzania imesema itahakikisha inaendelea kuimarisha hali ya ulinzi
na usalama kwa Watanzania na raia wa kigeni waliopo na wanaoendelea
kutembelea hapa nchini kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali
za binafsi na kimaendeleo ili watu wote waweze kutekeleza majukumu yao
na kuishi kwa amani na usalama nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema hayo jana wakati
akizungumza katika kikao baina yake na Ujumbe wa Wawakilishi wa nchi za
Umoja wa Ulaya na mabalozi wa nchi hizo hapa nchini kilichofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo.
Taarifa
ya wizara ilisema Nchimbi alisema kwa sasa Serikali kupitia polisi
imejiwekea mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu
katika Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
‘‘
Polisi tayari imeanzisha dawati maalumu litakalowahudumia raia wa
kigeni ili kuwawezesha kufungua kesi zao kwa urahisi, kuwapo kwa wepesi
wa majadiliano na ziweze kushughulikiwa kwa haraka na hatimaye kupatiwa
ufumbuzi”, alifafanua Waziri Nchimbi.
Waziri
Nchimbi alisema pia katika kusimamia suala la ulinzi na usalama wa raia
na mali zao kwa sasa wizara yake itafanya ukaguzi wa kampuni binafsi za
ulinzi ili kuangalia na kujiridhisha kama zinakidhi viwango vya ubora
vinavyotakiwa.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa Wawakilishi wa Nchi za Umoja wa Ulaya
hapa nchini, Balozi Filberto Cerani Sebregondi alisema umoja huo
utaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo pia
aliishukuru kwa jitihada inayoendelea kuchukua kuhakikisha ulinzi na
usalama kwa wageni na raia wa Tanzania unaimarika.
Kwa
upande wao mabalozi waliohudhuria kikao hicho waliitaka Serikali na
Watanzania kuhakikisha usalama unadumishwa ili kutoathiri taswira ya
Tanzania kimataifa na hivyo kuhatarisha uwezekaji na utalii.
Walisema
Umoja huo una imani na Serikali kwamba itaimarisha zaidi masuala ya
ulinzi na kuhakikisha raia wote wanalindwa kwa haki. CHANZO: MWANANCH