Baada ya
shutuma za rushwa ya ngono kuzidi kwa waandaaji wa shindano la Miss
Tanzania, uongozi unaosimamia shindano hilo umesema kama kuna mrembo
yeyote ambae amewahi kuombwa rushwa hiyo ya ngono ajitokeze.
Mkurugenzi
Hashim Lundenga amesema “kuna kushutumiwa kwamba tunachukua rushwa ya
ngono kutoka kwa Wasichana kitu ambacho sio kweli, hakuna msichana
aliesema ameingia kambini au ameshinda kwa sababu ametoa rushwa ya
ngono, katiba yetu inakataza kabisa yeyote kujihusisha na hilo”
Toka Miss
Tanzania ianze 1994 mpaka sasa kuna kesi zisizozidi nne za wazazi
waliokuja kuwaondoa watoto wao kwenye kushiriki mashindano hayo baada ya
kupata taarifa mbaya kuhusu hizo kashfa za ngono.
Moja ya
kesi hizo ni pamoja na ya Mchugaji aliemuondoa mwanae baada ya kupewa
ubalozi wa kinywaji chenye kilevi, mrembo mwingine alikua Nadya aliekua
masomoni Chuo kikuu familia yake ilikataa kabisa mtoto wao kushiriki.
Lundenga
amesema kuna wazazi wengine ambao walieleweshwa na wakaelewa akiwemo
Mzee Muhere ambae aliposikia mtoto wake ameshinda Miss Kinondoni
aliwapigia kelele sana lakini akaeleweshwa akaelewa na sasa mtoto wake
anamiliki kampuni kubwa na anaendesha maisha vizuri kuliko baba yake
alivyodhani.
Kwa
kumalizia, Lundenga amekiri kwamba wanao utaratibu, sheria na kanuni
kwenye katiba yao ambayo imepitishwa na Serikali ikiwa na maagizo
mablimbali ikiwemo marufuku ya kiongozi yeyote kuomba rushwa ya ngono.
Pamoja na
kuzushiwa hizo kashfa, amesema idadi ya Warembo wanaotaka kushiriki
haijapungua bali imeongezeka kwa sababu Wasichana ndio wanazidi
kujitokeza.