Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, May 6, 2013

SHAMBULIZI LA BOMU LAULA WANNE MOGADISHU.


 A Somali girl and her brother run to safety near the scene of a blast in Mogadishu April 14, 2013. At least 16 people were killed as two car bombs exploded outside the law courts in Somalia's capital Mogadishu and gunmen stormed the building on Sunday, be
Shambulizi la bomu MogadishuShambulizi la bomu Mogadishu.
MAAFISA wa Somalia wanakutana London kwa kongamano kuu Jumanne linaloleta pamoja washirika wa kimataifa kusaidia katika ujenzi mpya wa Somalia.

Takriban watu wanane waliuawa na wengine kadha kujeruhiwa katika shambulizi la bomu katika  mji mkuu wa Somalia, Mogadishu Jumapili. 

Shambulizi hilo limefanywa siku mbili kabla ya kongamano kuu mjini London linalolenga kutafuta uungaji mkono kwa Somalia kutoka kwa jamii ya Kimataifa.

Shambulizi hilo la  bomu lililenga eneo la K4 Kitongoji chenye shughuli nyingi katika mji huo m

kuu na kulenga msafara wa magari ya wajumbe waliokuwa ziarani kutoka Qatar. 

Polisi wanasema wajumbe hao waliepuka bila majeraha lakini wapita njia waliokuwa karibu waliuawa na wengine kujeruhiwa. Daktari aliyekuwa katika eneo la tukio hilo Mohamoud Yarow alisema uharibifu uliotokea ulikuwa mkubwa.

Kundi la wanamgambo  wa al-Shabab lenye ushirika na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida limekiri kufanya shambulio hilo. Na licha ya kudhoofishwa na vikosi vya ukanda huo, wanamgambo hao wameendelea kufanya mashambulizi ya hapa na pale.

Mwezi jana zaidi ya watu 30 waliuawa  wakati wanamgambo wa al-Shabab walipovamia jengo la mahakama ya juu mjini Mogadishu. Wiki jana serikali ilifunga baadhi ya barabara na kuweka vizuizi  kufuatia vitisho  katika mji huo mkuu. 


Kamanda wa  wilaya Abdi Mohamoud  Warsame alisema shambulizi la Jumapili  lingekuwa na maafa zaidi kama serikali isingeweka ulinzi mkali.

Maafisa wa Somalia wanakutana London kwa kongamano kuu Jumanne linaloleta pamoja washirika wa kimataifa kusaidia katika ujenzi mpya wa Somalia.  
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...