Mchezaji
wa mpira wa kikapu nchini Marekani mwenye asili ya Afrika Jason Collins
amejitangaza kuwa yeye ni shoga hatua ambayo imewashitua watu wengi
hususani wapenzi wa mchezo huo.
Jason Collins anakua mchezaji wa kwanza wa kimataifa mwanaume ambaye
bado anacheza mpira wa kikapu kutangaza kuwa ni shoga huku akisema kuwa
yeye ni mwanamme mweusi na ni shoga.
Rais wa Marekani Barack Obama amempongeza mwanababa huyo shoga mwenye
umri wa......miaka 34 anayecheza katika ligi ya NBA kwa kujitangaza hadharani. Rais Obama ambaye mwaka jana alitangaza kuunga mkono ndoa za mashoga alimpigia simu Collins na kumpongeza kwa ujasiri alioonyesha.



