
Amesema
mbinu hiyo mpya imeanza kutumiwa na majangili hao kwa muda mrefu sasa
na kwamba hivi sasa hawasafirishi pembe hizo zikiwa nzima nzima kwa kuwa
watakamatwa na vyombo vya usalama.
Mbowe
ameliambia Bunge kwamba hivi sasa, meno hayo hayasafirishwi tena kwa
meli kama zamani na badala yake kuna viwanda nchini ambavyo vinasaga
meno hayo na kisha kusafirishwa kama unga kupitia viwanja vya ndege vya
Tanzania.
Amefafanua
kwamba mtandao wa ujangili nchini unakua kila siku na kwamba watu
wanaofanya biashara hiyo wapo karibu na baadhi ya viongozi wa serikali
na wanajulikana na vyombo vya usalama.
Pamoja na kutaja kwamba kuna kiwanda cha kusaga pembe za ndovu, Mbowe hakukitaja kiwanda hic
ho.
Kamati
ya inayoshulika na masuala ya maliasili na utalii ya serikali na ambayo
inaongiozwa na wabunge imesema kwamba miaka saba ijayo tembo wote
watakuwa wamemalizika endapo serikali haitachukua hatua kali za
kuthibiti majangili wanaoihujumu sekta hiyo.
Mbowe ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya maliasili na utalii ya mwaka wa fedha 2014/14.
Wakati
akichangia Mbowe ameitaka serikali kuchukua hatua kali ili kudhibiti
majangili wa pembe za tembo kwa kuwa watu hao wabaya ambao
wanaliangamiza taifa.
“
Mheshimiwa mwenyekiti, naomba serikali ichukue hatua kali ikiwezekana
serikali majangili wote wanaohusika wanyongwe, wote wanyongwe, adhabu
hiyo itasaidia kukomesha mauji ya tembo wetu.