Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Tuesday, May 14, 2013

Mbio za Udiwani zikitarajiwa kuanza wiki ijayo mkoani Arusha Mwenyekiti CCM Themi akimbilia CUF...... Ripoti kamili hii hapa

Pichani ni aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Themi Petro Ndarivoi (Kulia) akirudisha kadi ya chama cha mapinduzi kwa mwenyekiti wa chama cha CUF halmashauri ya jiji la Arusha Hamza Mustaph kwenye makao makuu ya chama hicho jana jioni
Wakati kipenga cha uchaguzi wa udiwani kikitarajiwa kupilizwa wiki ijayo pichani ni Mwenyekiti wa CUF halmashauri ya jiji la Arusha Hamza Mustapha akimpatia kadi ya chama hicho Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Themi Petro Ndarivoi aliyejiunga na chama hicho jana jioni na kupewa fomu ya kugombea udiwani wa chama hicho kata ya Themi. (picha na Mahmoud Ahmad Arusha).

Mgombea udiwani kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF kata ya Themi kwenye uchaguzi utakaoanza wiki ijayo Petro Ndarivoi akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya CUF halmashauri ya jiji la Arusha jana jioni wakati aliporudisha rasmi kadi ya CCM na kuchukuwa kadi ya CUF mbele ya mgombea udiwani kwenye kata ya ELERAI John Bayo na mwenyekiti wa CUF wilaya ya Arusha Hamza Mustapha.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...