
MASKINI! Mwigizaji Idrissa Makupa ‘Kupa’ yuko katika wakati mgumu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Tabata General, jijini Dar baada ya kugundulika ana tatizo kwenye figo.
Kupa akiwa hospitali.
“Nilipopimwa zaidi nimegundulika kwenye figo kuna mawe madogomadogo,
mpaka sasa wanafanya utaratibu wa matibabu ili Mungu akijalia nipone,”
alisema Kupa ambapo mkewe, Mary anayemuuguza naye akionesha kuguswa na
tatizo hilo.“Yaani hapa nilipo hata chakula hakipiti, naomba Mungu amjalie mume wangu apone haraka,” alisema Mary.
Wawili hao walifunga ndoa siku chache zilizopita.