Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
akizungumza na balozi wa Canada nchini Tanzania Alexandre Leveque,
ofisini kwake Migombani.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiongozana na
balozi wa Canada nchini Tanzania Alexandre Leveque, baada ya mazungumzo
yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.Picha na Salmin Said-Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais-
--
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameihakikishia
Canada kuwa Zanzibar ina maeneo mazuri ya kuwekeza na kuwaomba
wawekezaji wa nchi hiyo kuja kuwekeza katika Nyanja tofauti zikiwemo
ujenzi wa hoteli kubwa za kitalii, kumbi za mikutano na uvuvi wa bahari
kuu.
Amesema
Zanzibar ina mahitaji makubwa ya uwekezaji katika maeneo hayo, na
kwamba hatua hiyo itasaidia kukuza uchumi wa taifa na kunyanyua kipato
cha wananchi.
Akizungumza
na balozi wa Canada nchini Tanzania balozi Alexandre Leveque ofisini
kwake Migombani, Maalim Seif amesema serikali imelenga kuweka mazingira
mazuri ya uwekezaji ili kuwawezesha wawekezaji wa ndani na nje kuja
kuwekeza miradi mbali mbali ya kiuchumi.
Aidha
Maalim Seif ameiomba nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kuleta wataalamu
wa Afya na walimu wa sayansi, ili kupunguza tatizo la wataalamu hao
nchini.
Amesema
licha ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta hizo, lakini bado zina
upungufu wa wataalamu wakiwemo madaktari wenye sifa, pamoja walimu wa
masomo ya sayansi.
Amesifu
mchango wa nchi hiyo hasa katika sekta za afya na elimu na kutaka
isichoke kutoa misaada yake katika kusaidia kunyanyua uchumi wa
Zanzibar.
Kwa
upande wake balozi Alexandre amesema Canada imekuwa ikihamasisha
wawekezaji binafsi, na kuahidi kuwahamisha kuja kuwekeza Zanzibar.
Kuhusu
upatikanaji wa wataalamu wa Afya na walimu wa Sayansi, balozi huyo
amesema atawasiliana na mamlaka zinazohusika, ili kupata wataalamu
wakiwemo wa kujitolea, watakaoweza kuja kufanya kazi katika maeneo hayo.
Amesema
Canada inajivunia uhusiano wa muda mrefu uliopo kati yake ya Zanzibar,
na kwamba uhusiano huo utaendelezwa kwa maslahi ya pande hizo mbili.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar



