Aliyekuwa mtu wa karibu sana na marehemu Sharo Milionea aliyefariki
dunia mwezi Septemba mwaka jana, Mussa Kitale alimaarufu kama Kitale
Rais wa Mateja leo kupitia mtandao wa kijamii wa facebook amewaomba wale
wapenzi na mashabiki wa marehemu Sharo Milionea wampigie kura ili
kumuwezesha marehemu Sharo kuchukua tuzo za Kilimanjaro Music Awards
2013 zilizopangwa kufanyika mwezi june mwaka huu.
Sharo Milionea amebahatika kuingia katika vipengele viwili kwenye
kuwania tuzo hizo, (1) Wimbo bora wa Pop (2) Wimbo bora wa
kushirikishwa. Hivyo basi ili kumfanikisha marehemu Sharo kunyakuwa tuzo
ya kipengele (1) andika BP3 kisha tuma kwenda 15345, na kumuwezesha
kushinda kipengele (2) andika BR1 kisha tuma kwenda 15345.