Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Wednesday, May 15, 2013

HII NDIO KAULI YA WEMA SEPETU BAADA YA PICHA YAKE NA RAHEEM KUSAMBAA MITANDAONI


Mwanadada Wema Sepetu ambaye amabaye kipindi cha nyuma kama utakuwa mfuatiliaje mzuri wa habari zetu utakuwa umeeonah picha yake ambayo alikuwa ametokelezea na mwanaume amabye  aliyetajwa kwa jina moja la Raheem katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Baada ya habari hii  kuvuma sana mitandaoni  gazeti kongwe hapa nchini   lilimtafuta Raheem ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha.
Raheem alikiri kuitambua picha yake na Wema lakini alisema imemshtua na kumcha-nganya maana hakutegemea kama ingefika mitandaoni na hatimaye kwenye vyombo vya habari alifunga kama hivi 

“Ni kweli nilipiga hiyo picha na Wema lakini ni ya kawaida tu, haina maana nyingine tofauti. Wema ni rafiki yangu na dada yangu. Tunaheshimiana, hakuna cha zaidi.
“Wema ni maarufu na watu wanaweza kujaji wanavyotaka, hilo litanisababishia matatizo kwa sababu mimi nina mpenzi wangu na Wema si mtu wangu kabisa...she is just my sister (ni dada yangu tu).”
Mwandishi: Hiyo picha mlipiga lini, wapi na kwa matumizi gani?
Raheem: Ilikuwa kwenye function (tukio) fulani ambayo siwezi kuizungumzia. Kama wiki sita au miezi miwili hivi iliyopita na tulipiga kama marafiki tu, hakuna cha zaidi.
Risasi: Kwa hiyo Wema akithibitisha wewe ni mpenzi wake itakuwaje?
Raheem: Nitamshangaa sana! Wema ni dada yangu tu.
mwandishi: Inasemekana Wema ameamua kuianika hiyo picha kwa lengo la kumrusha roho Diamond, unasemaje hapo?
Raheem: Sijui na kwa kweli siwezi kuzungumzia mambo ya mtu binafsi. Sijui chochote.


Pia kwa upande wa Wema  alikiri kupiga picha na Raheem, akafafanua kuwa aliipiga muda mfupi baada ya kutoka kufanya interview na kituo kimoja cha redio (jina kapuni) lakini akasema haina uhusiano wowote na suala la mapenzi.

“Ni kweli nilipiga hiyo picha, yeye aliniomba tu kama fan (shabiki) wangu, akataka ku-show love (kuonesha upendo), sikuona sababu ya kumkatalia. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Martin (Kadinda – meneja wake) na baada ya siku hiyo sijawahi kuonana naye tena mahali popote...sioni tatizo kabisa, ni kawaida kwa sisi mastaa,” alisema Wema.
Mwandishi: Lakini Wema wadau wanasema eti ni mpenzi wako na umefanya hivyo kwa lengo la kumrusha roho Diamond.
Wema: Umeshasema wadau, waache na mambo yao lakini maelezo yangu ni hayo na naamini yamejitosheleza.
Mwandishi: Kuna kitu nahitaji ufafanue zaidi...lile pozi lipo romantic sana, hufikiri kuwa inaweza kuwa sababu ya watu kuwa na hisia kwamba ni mpenzi wako?
Wema: Ni kweli picha ni romantic lakini yule kijana (Raheem) si mpenzi wangu. Naomba nieleweke hivyo. Ahsante.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...