Baada
ya kutumikia kifungo cha karibu miaka miwili jela, hatimaye rapper
Ja-Rule ameachiwa. Ja Rule alikuwa jela kwa makosa ya kukwepa kulipa
kodi na kumiliki silaha.
Ameachiwa miwezi miwili kabla ya muda kwenye gereza la Ray Brook
jijini New York jana. Rapper huyo alipokelewa na mke wake na kuelekea
nyumbani ambako atakuwa kwenye ‘house arrest’ hadi July 28.