Maisha ya wakazi wa mijini na majijini na maeneo mengine yanayokuwa na hata vijijini yapo hatarini kiafya, kutokana na kutumia vinywaji vinavyohifadhiwa kwenye chupa hususan za plasiti zilizotumika.

Chupa hizo ni zile zilizotumiwa na watu tofauti, kisha kutupwa ambapo zinaokotwa na kuuzwa kwa wahitaji wanaozitumia kuhifadhia vinywaji vya aina tofauti.

Kutokana na mazingira hayo, watu wengi wapo kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa ya milipuko kama kuharisha, kipindupindu na kifua kikuu.

Uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa afya ya

Mazingira,
umebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa vinywaji kama maji baridi, juisi za aina tofauti, wanatumia chupa zilizotumika, kuhifadhi vinywaji hivyo.

Hata hivyo, hali hiyo ipo zaidi kwa wafanyabiashara katika maeneo yanayokaliwa na watu wenye hali duni kiuchumi, hivyo mahitaji ya vinywaji hivyo vinavyouzwa kwa bei ndogo kuwa makubwa.

Maeneo ambayo yamebainika kuwa na wateja wengi wa bidhaa hizo kuwa ni shule za msingi na sekondari, sokoni, maeneo ya viwanda, vituo vya daladala na kwenye makazi duni.






Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam, anasema chupa hizo ni chafu na hazifai kwa matumizi yaliyozoeleka kwa baadhi ya wananchi.

Anasema tatizo la watu kuuza vinywaji vinavyohifadhiwa kwenye chupa hizo, limekuwa sugu majiji na maeneo mengine ya nchi.

Anasema matumizi hayo si sahihi kwa vile, chupa hizo si salama na kwamba watu wanaweza kupata magonjwa ya tumbo, kuharisha na kipindupindu.

Anasema pia endapo mtu aliyetumia chupa hizo ana ugonjwa wa kifua kikuu, ni rahisi kwa mtu anayeitumia kwa mara ya pili kuathirika kwa ugonjwa huo.



Watalaam wa afya ya mazingira anasema kitendo cha watu kuokota chupa zilizotumika na kuhifadhi bidhaa zao, kinapaswa kupigwa vita ili kunusuru maisha ya watu.

Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke anasema ameshashuhudia watu `wanavyovamia’ maeneo ya viwanja vya soka vya Taifa na Uhuru baada ya mechi za mpira wa miguu kumalizika, wakiokota chupa zilizotumika.

Anasema mara nyingi mashabiki wengi wanakosa ustaarabu, kiasi cha kutumia chupa za maji kuhifadhi haja ndogo, jambo linalochangia kuhalalisha kuwa chupa hizo hazipo salama.

"Mimi naingia mara nyingi kwenye viwanja vile kuangalia mpira, baada ya mechi, chupa nyingi utaziona zina mikojo na watu wanaziokota, bila shaka ni miongoni mwa zinazotumika kuhifadhia vinywaji kwa mara ya pili,” anasema.

Hata hivyo, Inathibitisha kuwepo kwa hali hiyo, na kufafanua kwamba chupa `zinazozalishwa’ na mashabiki wa mpira, ni kero dhidi ya usafi wa mazingira katika eneo hilo na hata katika maeneo mengine yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.



WANAFUNZI HATARINI

Katika uchunguzi wa wataalamu wa sayansi ya afya ya mazingira,

imebainika kada iliyo katika hatari zaidi ya kuathirika kutokana na matumizi ya chupa hizo ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Katika baadhi ya shule zilizotembelewa katika maeneo tofauti ya mijini na vijijini,

wanafunzi walionekana wakinunua kwa
wingi juisi hizo na kunywa bila kujali kama usafi wake.
Baadhi ya shule zilizoonekana kushamiri kwa biashara.


Walimu wanasema tatizo hilo limekuwa kubwa, likichochewa na wafanyabiashara wanaowalenga wanafunzi kuwa soko la bidhaa zao.

Walimu wanasema baada ya kutoa waraka maalum wa kuzuia biashara hiyo, wengi wa wafanyabiashara wanauzia nyumbani, hivyo ni vigumu kuwafuata na kuwazuia.

Mwalimu wa Afya wa Shule ya moja Msingi niliemuuliza anasema shule yake pamoja na kupiga marufuku biashara hizo, bado watu wanaingiza kinyemela na kuwauzia wanafunzi.

"Hivi karibuni tumekaa na wafanyabiashara tuliawaambia hatutaki bidhaa zinazohifadhiwa kwenye chupa au vifaa vilivyotumika, wengi wamekubali lakini wapo wanaokaidi," anasema Mwalimu huyo.



WAFANYABIASHARA WAJITETEA

Baadhi ya wafanyabiashara wanaouza juisi ya miwa na ya matunda mengine kwa kutumia chupa zilozotumika, wamesema hawahatarishi afya za binadamu kwa sababu wanazisafisha kwa kufuata kanuni ya afya.

Wanasema wengi wao wanajua umuhimu wa afya na ndio maana wanapopata chupa hizo, wanazisafisha kwa maji ya moto pamoja na sabuni.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, anasema awali alihifadhi juisi aliyoitengeneza kwenye mifuko maalum ya plastiki, lakini alikuwa akipungukiwa na wateja kutokana na ugumu wa utumiaji wake.

"Chupa za maji ni nzuri sana hata wateja wetu, wanazipenda na ndio maana wengi tumeacha kuuza kwenye mifuko ya plastiki," anasema.

Mfanyabiashara mwingine, anasema baadhi yao wameshindwa kufuata kanuni za afya, hivyo kuwasababishia wengi wao kujikuta wakiingia kwenye kashfa ya bidhaa chafu.

Nakushauri wewe mtumiaji au Mpenzi wa

Kutumia vinywaji vilivyowekwa kwenye
Chupa ambazo zimekishwa tumika achana nazo kwa ajiri ya afya yako si salama hata kidogo.
Unaweza onani za bei rahisi tu lakini madhara yake ni makubwa ambayo yanaweza kukugharimu maisha yako pale magonjwa yatakapo kupata.
Wazazi na walezi wenye watoto wanaoenda shule, ni vyema mkawashauri kwa kuwaelimisha athari za bidhaa hizo ni vyema kuwapatia kama ni jiusi au vinywaji vingine toka nyumbani ambayo watatumia wakiwa maeneo ya shule. chanzo. ManyandaHealthy